Mpya

Doumbia akiri anapitia wakati mgumu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Sep 2026
Doumbia akiri anapitia wakati mgumu

Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Doumbia, amekiri kuwa anapitia kipindi kigumu cha kutofunga mabao katika hatua za mwanzo za msimu, akisema hali hiyo ni mpya kwake tangu aanze kucheza soka la ushindani.

Doumbia amesema licha ya kupata nafasi za kucheza, bado hajafanikiwa kupata bao, jambo ambalo amelitaja kuwa sehemu ya changamoto za mchezo wa soka, hasa msimu unapokuwa umeanza.

“Ni mara ya kwanza kabisa kwangu kupitia kipindi cha aina hii, kwa sababu hii ni ligi ambayo ndiyo kwanza imeanza. Kwa hiyo ni jambo la kawaida, hasa unapokuwa unapata nafasi yako ya kwanza. Hivyo, hii ni mara yangu ya kwanza kupitia hali kama hii,” amesema Doumbia.

Doumbia anaamini hali hiyo ni sehemu ya mchakato wa msimu na kwamba kupata nafasi za kufunga ni hatua muhimu kabla ya mabao kuanza kupatikana.

Kauli ya Doumbia inakuja wakati Wanasimba wakiendelea kump sapoti huku benchi la ufundi chini ya kocha Steve Barker akionyesha kuwa na imani nae licha ya changamoto inayomkabili.

Licha ya kutofunga, Doumbia anaonekana kuwa ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa akidhihirisha hilo dakika chache alizocheza kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mighty Wonderers.

More Stories

Karibu Azam Complex kwenye show za Libasse Gueye
Karibu Azam Complex kwenye show za Libasse Gueye
29m ago
READ MORE β†’
Mzizima Derby; Azam Fc vs Simba leo
Mzizima Derby; Azam Fc vs Simba leo
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Azam Fc yamekamlika
Maandalizi ya kuikabili Azam Fc yamekamlika
15h ago
READ MORE β†’
Hatuhitaji kupoteza mchezo dhidi ya Azam Fc - Barker
Hatuhitaji kupoteza mchezo dhidi ya Azam Fc - Barker
1d ago
READ MORE β†’
Mzizima Derby haijawahi kuwa nyepesi
Mzizima Derby haijawahi kuwa nyepesi
1d ago
READ MORE β†’
Kituo kinachofuata ni MZIZIMA DERBY
Kituo kinachofuata ni MZIZIMA DERBY
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Septemba 15 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Septemba 15 2026
1d ago
READ MORE β†’
Doumbia bado kidogo, Mgunda akosha mashabiki
Doumbia bado kidogo, Mgunda akosha mashabiki
1d ago
READ MORE β†’
Tulitaka kutuma ujumbe Afrika - Ahmed
Tulitaka kutuma ujumbe Afrika - Ahmed
1d ago
READ MORE β†’