Mpya

Mighty Wonderers kutua nchini leo, Simba yawaandalia dozi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1d ago
Mighty Wonderers kutua nchini leo, Simba yawaandalia dozi

Wapinzani wa Simba Mighty Wonderers wanatarajiwa kuwasili nchini leo kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa utakaopigwa Jumapili.

Mchezo huo wa mkondo wa pili hatua ya awali ya michuano hiyo, utapigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Mighty wanatua nchini huku wakiwa tayari wako nyuma kwa bao 1-0 wakipokea kipigo kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa nchini Malawi.

Wakati timu ikitarajiwa kuwasili leo, Wekundu wa Msimbazi wanaendelea na maandalizi yao Mo Simba Arena kuelekea mchezo huo.

Baada ya ushndi ugenini Simba inahitaji ushindi mwingine au hata matokeo ya sare kwenye mchezo huo ili kutinga raundi ya kwanza.

Kikosi cha kocha Steve Barker kimedhamiria kumaliza kazi mapema pale uwanja wa Uhuru siku ya Jumapili mchezo huo ukitarajiwa kupigwa mbele ya mashabiki wa Simba.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amewataka mashabiki wa timu hiyo kuendelea kununua tiketi kwa wingi ili kuhakikisha wanaujaza uwanja wa Uhuru siku ya Jumapili.

More Stories

Simba yakamilisha maandalizi dimba la Uhuru
Simba yakamilisha maandalizi dimba la Uhuru
4h ago
READ MORE β†’
Libasse ameweka kabatini tuzo ya kwanza ya ligi kuu msimu huu
Libasse ameweka kabatini tuzo ya kwanza ya ligi kuu msimu huu
7h ago
READ MORE β†’
Mighty Wonderes wawasili Dar usiku
Mighty Wonderes wawasili Dar usiku
10h ago
READ MORE β†’
Makgalwa ajipa muda zaidi Simba
Makgalwa ajipa muda zaidi Simba
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Septemba 11 2026
14h ago
READ MORE β†’
Kibabage ameanza mazoezi mepesi
Kibabage ameanza mazoezi mepesi
1d ago
READ MORE β†’
Chama apotezea kelele za mitandaoni, aweka msimamo
Chama apotezea kelele za mitandaoni, aweka msimamo
1d ago
READ MORE β†’
Oura anaamini huu utakuwa msimu bora kwa Simba
Oura anaamini huu utakuwa msimu bora kwa Simba
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Septemba 10 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Septemba 10 2026
1d ago
READ MORE β†’