Mlinzi wa kushoto wa Simba Nickson Kibabage ameanza mazoezi mepesi ikiwa ni hatua muhimu kuelekeaa kuimarisha majeraha aliyopata.
Kibabage alipata majeraha ya nyama za paja katika mguu wake wa kulia kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar.
Tayari amekosekana uwanjani kwa takribani wiki tatu lakini sasa akianza hatua muhimu ya kuimarika kabla ya kurejea tena uwanjani.
Kibabage ameungana na Abdulrazak Hamza na Wilson Nangu ambao pia wanaendelea na program maaum za mazoezi kabla ya kurejea rasmi kwenye majukumu yao.
Nangu na Hamza wamekosekana kwa takribani msimu mzima sasa baada kupata majeraha ambayo yalipelekea wafanyiwe upasaji.

