Timu ya Mighty Wonderers ya Malawi imewasili nchini kuelekea mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya wenyeji wao Simba.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumapili, Septemba 13 katika uwanja wa Uhuru.
Simba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0 ambao walipata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza nchini Malawi.
Wekundu hao wa Msimbazi watahitaji ushindi au matokeo yoyote ya sare ili kutinga raundi ya kwanza.