Kiungo mshambuliaji wa Simba Libasse Gueye ametangazwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya NBC kwa mwezi August 2026.
Libasse ametwaa tuzo hiyo baada ya kuonyesha kiwango kizuri mwezi August ambapo alihusika kwenye mabao sita yaliyofungwa na Simba.
Alitoa pasi tano za mabao huku pia akifunga bao moja. Katika kinyang'anyiro hicho amewashinda Maxi Nzengeli wa Yanga na Oscar Mwajanga wa Mbeya City.
