Mpya

Hatubweteki na ushindi wa mechi ya kwanza - Barker

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4d ago
Hatubweteki na ushindi wa mechi ya kwanza - Barker

Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amesema ushindi wa bao 1-0 walioupata dhidi ya Mighty Wanderers ya Malawi katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) haujawafanya kujiona tayari wameshamaliza kazi.

Barker amesisitiza kuwa wanahitaji kuonyesha kiwango bora zaidi katika mchezo wa marudiano.

Simba iliibuka na ushindi ugenini katika mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Malawi, matokeo ambayo yameiweka katika nafasi nzuri kuelekea mchezo wa pili utakaopigwa kesho Jumapili, Septemba 13, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Barker amesema ushindi wa ugenini ni matokeo muhimu, lakini kikosi chake hakitakiwi kubweteka kwa faida hiyo, badala yake kinapaswa kuongeza kiwango mbele ya mashabiki wake.

“Tunahitaji kuonyesha kiwango zaidi mbele ya mashabiki wetu. Malengo ni kushinda na kwenda hatua inayofuata, ambayo itatupa nafasi ya kupigania hatua ya makundi msimu huu,” amesema Barker.

Barker amesema dhamira ya Simba ni kuhakikisha inapata matokeo yatakayoipa nafasi ya kusonga mbele katika mashindano hayo, huku ikilenga kufika hatua ya makundi msimu huu.

Libasse Gueye Arejea

Wakati huo huo, Barker amesema kurejea kwa mshambuliaji Libasse Gueye, ambaye alikosekana katika mchezo wa kwanza dhidi ya Mighty Wanderers, kumeongeza morali ndani ya kikosi.

Kocha huyo ameeleza kuwa uwepo wa Gueye ni nyongeza muhimu kwa timu kutokana na umuhimu wake katika mipango ya kiufundi ya Simba.

Simba itashuka dimba la Uhuru hapo kesho ikisaka matokeo yatakayoiwezesha kutinga raundi inayofuata ya CAFCL na kuendelea na safari ya kuwania nafasi ya kucheza hatua ya makundi.

More Stories

Karibu Azam Complex kwenye show za Libasse Gueye
Karibu Azam Complex kwenye show za Libasse Gueye
29m ago
READ MORE β†’
Mzizima Derby; Azam Fc vs Simba leo
Mzizima Derby; Azam Fc vs Simba leo
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Azam Fc yamekamlika
Maandalizi ya kuikabili Azam Fc yamekamlika
15h ago
READ MORE β†’
Hatuhitaji kupoteza mchezo dhidi ya Azam Fc - Barker
Hatuhitaji kupoteza mchezo dhidi ya Azam Fc - Barker
1d ago
READ MORE β†’
Mzizima Derby haijawahi kuwa nyepesi
Mzizima Derby haijawahi kuwa nyepesi
1d ago
READ MORE β†’
Kituo kinachofuata ni MZIZIMA DERBY
Kituo kinachofuata ni MZIZIMA DERBY
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Septemba 15 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Septemba 15 2026
1d ago
READ MORE β†’
Doumbia bado kidogo, Mgunda akosha mashabiki
Doumbia bado kidogo, Mgunda akosha mashabiki
1d ago
READ MORE β†’
Tulitaka kutuma ujumbe Afrika - Ahmed
Tulitaka kutuma ujumbe Afrika - Ahmed
1d ago
READ MORE β†’