Mpya

Chama na rekodi ya kutisha ya mabao ligi ya mabingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1d ago
Chama na rekodi ya kutisha ya mabao ligi ya mabingwa

Kiungo Clatous Chama jana aliendeza makali yake kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika akiwaongoza Wekundu wa Msimbazi kuibuka na ushindi wa mabao 6-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo ambao Simba iituma salamu kwa wapinzani wake kwenye ligi ya mabingwa msimu ikishinda kwa jumla ya mabao 7-1 katika mechi zote mbili, Chama aliweka kambani mabao mawili.

Mabao hayo yamemfanya Chama kuendeleza rekodi yake nzuri katika michuano hiyo akisogea hadi nafasi ya tano katika vinara wa mabao wa muda wote wa ligi ya mabingwa.

Chama amefikisha mabao 24 akiwa nyuma kwa tofauti ya mabao saba dhidi ya kinara wa muda wote Mohamed Aboutrika aliyefunga mabao 31.

Katika mabao hayo, 19 ameyafunga akiwa na klabu ya Simba, mabao matatu aliyafunga akiwa na Yanga na mabao mawili aliyafunga akiwa na Zesco United ya kwao Zambia.

Klabu ya Simba SC ndiyo inayoshikilia sehemu kubwa ya mafanikio ya Chama kiufungaji. Akiwa na Wekundu wa Msimbazi, "Mwamba wa Lusaka" amepachika jumla ya mabao 19. Miongoni mwa magoli yake bora akiwa na Simba ni magoli ya dakika za mwisho yaliyoipeleka Simba hatua ya robo fainali, kama vile goli dhidi ya Nkana FC na AS Vita Club (msimu wa 2018/19 na 2020/21).

Baada ya kurejea tena Simba, Chama ameendeleza makali yake kwa kufunga mabao mawili (brace) jana katika ushindi mnono wa 6-1 dhidi ya Mighty Wanderers ya Malawi. 

More Stories

Karibu Azam Complex kwenye show za Libasse Gueye
Karibu Azam Complex kwenye show za Libasse Gueye
30m ago
READ MORE β†’
Mzizima Derby; Azam Fc vs Simba leo
Mzizima Derby; Azam Fc vs Simba leo
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Azam Fc yamekamlika
Maandalizi ya kuikabili Azam Fc yamekamlika
15h ago
READ MORE β†’
Hatuhitaji kupoteza mchezo dhidi ya Azam Fc - Barker
Hatuhitaji kupoteza mchezo dhidi ya Azam Fc - Barker
1d ago
READ MORE β†’
Mzizima Derby haijawahi kuwa nyepesi
Mzizima Derby haijawahi kuwa nyepesi
1d ago
READ MORE β†’
Kituo kinachofuata ni MZIZIMA DERBY
Kituo kinachofuata ni MZIZIMA DERBY
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Septemba 15 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Septemba 15 2026
1d ago
READ MORE β†’
Doumbia bado kidogo, Mgunda akosha mashabiki
Doumbia bado kidogo, Mgunda akosha mashabiki
1d ago
READ MORE β†’
Tulitaka kutuma ujumbe Afrika - Ahmed
Tulitaka kutuma ujumbe Afrika - Ahmed
1d ago
READ MORE β†’