Mpya

Doumbia bado kidogo, Mgunda akosha mashabiki

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1d ago
Doumbia bado kidogo, Mgunda akosha mashabiki

Jana mshambuliaji wa Simba Ibrahim Doumbia alikuwa sehemu ya kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi walioibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya Mighty Wonderers katika mchezo wa mkondo wa pili hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL).

Simba iligawa dozi nene ikiondoka na ushindi wa jumla wa mabao 7-1 kufuatia ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza.

Bado Wanamsimbazi wanasubiri kushangilia bao la kwanza la Doumbia kwenye mechi za mashindano kwani kwa mara nyingine hakufanikiwa kuweka mpira kambani licha ya kutengenezewa nafasi kadhaa.

Jambo la uhakika ni kuwa, ni suala la muda tu Wanasimba watashangilia bao la mshambuliaji huyo kutoka Mali.

Katika mchezo huo pia kocha Steve Barker alimpa nafasi mshambuliaji Ismail Mgunda aliyesajiliwa kuchukua nafasi ya Suleiman Mwalimu aliyetimkia Yanga siku moja kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Mgunda alionyesha kiwango kizuri kwa muda mchache aliocheza akiongeza imani kwa Wanamsimbazi kuwa anaiweza kuifanya vyema kazi ya kuongoza safu ya ushambuliaji.

Mashabiki wa Simba wameendelea kuwaunga mkono washambuliaji hao ili kuhakikisha hawaondolewi mchezoni na presha za nje ya uwanja.

Doumbia kwa sasa anaonekana kufurahia zaidi sapoti anayopewa na mashabiki wa Simba, jambo linalomuongezea kujiamini.

More Stories

Karibu Azam Complex kwenye show za Libasse Gueye
Karibu Azam Complex kwenye show za Libasse Gueye
29m ago
READ MORE β†’
Mzizima Derby; Azam Fc vs Simba leo
Mzizima Derby; Azam Fc vs Simba leo
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Azam Fc yamekamlika
Maandalizi ya kuikabili Azam Fc yamekamlika
15h ago
READ MORE β†’
Hatuhitaji kupoteza mchezo dhidi ya Azam Fc - Barker
Hatuhitaji kupoteza mchezo dhidi ya Azam Fc - Barker
1d ago
READ MORE β†’
Mzizima Derby haijawahi kuwa nyepesi
Mzizima Derby haijawahi kuwa nyepesi
1d ago
READ MORE β†’
Kituo kinachofuata ni MZIZIMA DERBY
Kituo kinachofuata ni MZIZIMA DERBY
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Septemba 15 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Septemba 15 2026
1d ago
READ MORE β†’
Tulitaka kutuma ujumbe Afrika - Ahmed
Tulitaka kutuma ujumbe Afrika - Ahmed
1d ago
READ MORE β†’