Mpya

Kituo kinachofuata ni MZIZIMA DERBY

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1d ago
Kituo kinachofuata ni MZIZIMA DERBY

Baada ya kujihakikishia kutinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa kibabe kwa ushindi wa jumla wa mabao 7-1 dhidi ya Mighty Wonderers, kikosi cha Simba kimeelekeza nguvu zake kwenye ligi.

Kesho Jumatano, Septemba 16 Simba itashuka uwanja wa Azam Complex, kuikabili Azam Fc katika mchezo wa mzunguuko wa sita ligi kuu ya NBC.

Ni Derby ya Mzizima mechi itakazozikutanisha timu mbili zenye ushindani wa aina yake unaotokana na historia.

Kabla ya kuanzisha rasmi klabu ya Azam FC, bilionea na mfanyabiashara maarufu Said Salim Bakhresa aliwahi kuwa mmoja wa wafadhili wakubwa waliounga mkono na kutoa huduma au kwa klabu ya Simba SC kupitia ofisi zilizokuwa katika eneo hilo la Mzizima. 

Baada ya kuibuka mvutano wa kiuongozi na kifedha, uwekezaji huo ulijiondoa Simba na kuamua kuanzisha timu mpya ambayo sasa ni Azam Fc.

Kwa misimu ya karibuni, Azam Fc imekuwa timu ngumu kufungika na Simba hasa zinapokutana kwenye ligi.

Msimu uliopita Simba iliambulia alama moja tu baada ya suluhu ya bila kufungana na mchezo wa raundi ya pili wa ligi huku Azam Fc wakichukua alama nne.

Hata hivyo mara ya mwisho timu hizo zilikutana kwenye fainali ya kombe la CRDB Simba ikiibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0 na kutwaa taji hilo.

Msimu huu Simba imeweka malengo makubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi hivyo ushindi dhidi ya Azam Fc yatakuwa matokeo muhimu zaidi kwa Simba.

More Stories

Karibu Azam Complex kwenye show za Libasse Gueye
Karibu Azam Complex kwenye show za Libasse Gueye
29m ago
READ MORE β†’
Mzizima Derby; Azam Fc vs Simba leo
Mzizima Derby; Azam Fc vs Simba leo
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Azam Fc yamekamlika
Maandalizi ya kuikabili Azam Fc yamekamlika
15h ago
READ MORE β†’
Hatuhitaji kupoteza mchezo dhidi ya Azam Fc - Barker
Hatuhitaji kupoteza mchezo dhidi ya Azam Fc - Barker
1d ago
READ MORE β†’
Mzizima Derby haijawahi kuwa nyepesi
Mzizima Derby haijawahi kuwa nyepesi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Septemba 15 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Septemba 15 2026
1d ago
READ MORE β†’
Doumbia bado kidogo, Mgunda akosha mashabiki
Doumbia bado kidogo, Mgunda akosha mashabiki
1d ago
READ MORE β†’
Tulitaka kutuma ujumbe Afrika - Ahmed
Tulitaka kutuma ujumbe Afrika - Ahmed
1d ago
READ MORE β†’