Mpya

Mzizima Derby haijawahi kuwa nyepesi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1d ago
Mzizima Derby haijawahi kuwa nyepesi

Ligi Kuu ya NBC kesho inatarajia kushuhudia miamba miwili ya soka jijini Dar es salaam, Azam FC na Simba SC, itakapovaana katika dabi ya kukata na shoka maarufu kama 'Mzizima Derby', itakayopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Mchezo huo unakuja huku Simba ikiwa na hesabu kali za pointi tatu ili kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi. Lakini mchezo baina ya timu hizo haujawahi kuwa mwepesi kwani  timu zote mbili zimekuwa zikipishana vikali.

Rekodi zinasemaje?

Takwimu kutoka mechi 10 zilizopita za Ligi Kuu baina ya timu hizi zinaonesha kuwa hakuna mbabe wa wazi, jambo linalofanya mchezo wa kesho kutabirika kwa ugumu mkubwa.

Katika mapambano 10 yaliyopita, Simba SC imefanikiwa kuondoka na ushindi mara tatu (3), huku matajiri wa Chamazi, Azam FC, wakishinda mara mbili (2). Miamba hii imetoka sare katika michezo mitano (5).

Mechi ya mwisho kukutana ilikuwa Aprili 5, 2026, ambapo timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya 0-0 kwenye uwanja huo huo wa Chamazi.

Hata hivyo, Azam FC wataingia uwanjani wakikumbuka ushindi wao wa mabao 2-0 walioupata ugenini dhidi ya Simba mnamo Desemba 7, 2025.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema safari hii Simba imejipanga kuhakikisha haipotezi alama dhidi ya Azam Fc.

"Azam Fc ni miongoni mwa timu ambazo zimekuwa zikituvurugia hesabu zetu kwenye mbio za ubingwa, safari hii tumejipanga hatutaki kudondosha alama dhidi yao," alisema Ahmed.

Simba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na takwimu bora zaidi msimu huu kwani Wekundu hao wa Msimbazi wameshinda mechi zote tano za ligi kuu na mechi mbili za ligi ya mabingwa huku Azam Fc wakiwa tayari wamedondosha alama nne kwenye ligi.

More Stories

Karibu Azam Complex kwenye show za Libasse Gueye
Karibu Azam Complex kwenye show za Libasse Gueye
29m ago
READ MORE β†’
Mzizima Derby; Azam Fc vs Simba leo
Mzizima Derby; Azam Fc vs Simba leo
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Septemba 16 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Azam Fc yamekamlika
Maandalizi ya kuikabili Azam Fc yamekamlika
15h ago
READ MORE β†’
Hatuhitaji kupoteza mchezo dhidi ya Azam Fc - Barker
Hatuhitaji kupoteza mchezo dhidi ya Azam Fc - Barker
1d ago
READ MORE β†’
Kituo kinachofuata ni MZIZIMA DERBY
Kituo kinachofuata ni MZIZIMA DERBY
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Septemba 15 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Septemba 15 2026
1d ago
READ MORE β†’
Doumbia bado kidogo, Mgunda akosha mashabiki
Doumbia bado kidogo, Mgunda akosha mashabiki
1d ago
READ MORE β†’
Tulitaka kutuma ujumbe Afrika - Ahmed
Tulitaka kutuma ujumbe Afrika - Ahmed
1d ago
READ MORE β†’