Licha ya muda mchache wa maandalizi, Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa kesho Jumatano kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam.
Akizungumzia maandalizi kuelekea mchezo huo, Barker alisema wamekuwa na muda mfinyu wa maandalizi kutoka mechi iliyopita hata hivyo wanafahamu umuhimu wa mchezo huo.
Barker amesema ili Simba kufikia malengo yake ya msimu huu, mchezo huo ni miongoni mwa mechi ambazo wanahitaji kushinda.
"Tumekuwa na muda mchache wa maandalizi tangu tulipocheza mchezo wa mwisho ila mechi ya kesho ni muhimu sana kwetu."
"Tunahitaji kupata ushindi ili tulinde malengo yetu ya msimu huu. Kama unakumbuka msimu uliopita tulipoteza pointi nne dhidi ya yao."
"Tunataka kuwa bora na kufanya vizuri zaidi msimu huu," alisema Barker