Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2d ago
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki

Kocha Mkuu wa Simba SC, Steven Barker, ameweka wazi msimamo wake kuelekea mchezo dhidi ya FC 15 de Agosto de Akonibe, akitaka kikosi chake kiwe tayari kupambana na kutafuta ushindi licha ya kucheza bila mashabiki mchezo wa mkondo wa kwanza.

Simba inatarajiwa kukutana na timu hiyo kutoka Guinea ya Ikweta katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika, utakaochezwa Jumatano, Oktoba 21, saa 9 jioni kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Hata hivyo, mchezo huo unatarajiwa kuchezwa bila mashabiki kufuatia ombi lililotolewa na wawakilishi wa 15 de Agosto wakati wa maandalizi ya mechi hizo mbili.

"Uwepo wa mashabiki ni sehemu muhimu ya nguvu ya Simba, hasa katika michezo mikubwa ya kimataifa inayohitaji ari, kujituma na kujiamini kwa wachezaji"

"Wanasimba wamekuwa na mchango mkubwa katika kuipa timu hii hamasa inapokuwa uwanjani, hivyo kutokuwepo kwao kutakuwa changamoto kidogo lakini hali hiyo haitabadilisha dhamira yetu ya kupigania matokeo mazuri," alisema

Licha ya kutoridhishwa na uwezekano wa kucheza mbele ya viti visivyo na mashabiki, Barker amewataka wachezaji wake waelekeze nguvu zao katika kutekeleza majukumu yao ndani ya uwanja badala ya kuruhusu mazingira ya mchezo kuathiri maandalizi yao.

Simba inaingia katika hatua hii ikiwa na matokeo mazuri kutoka raundi iliyopita, baada ya kuiondoa Mighty Wanderers ya Malawi kwa jumla ya mabao 7-1.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa ugenini Septemba 6, Wekundu wa Msimbazi walipata ushindi wa bao 1-0 kabla ya kuendeleza ubabe wao katika mchezo wa marudiano kwa kuibuka na ushindi wa mabao 6-1.

Matokeo hayo yaliipa Simba nafasi ya kuendelea na safari yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini sasa inakabiliwa na mtihani mpya dhidi ya 15 de Agosto.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
2h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
6h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
20h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
1d ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 18 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 18 2026
2d ago
READ MORE β†’