Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1d ago
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano

Kikosi cha Simba kinaendelea na maandalizi yake Mo Simba Arena kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa (CAFCL) dhidi ya 15 de Agosto ya Guinea ya Ikweta.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa siku ya Jumatano, Oktoba 21 kwenye uwanja wa Uhuru, de Agosto wakiwa wenyeji.

Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker ameweka wazi mkakati wa Wekundu hao wa Msimbazi ni kupata ushindi kwenye mchezo huo wa kwanza ili kupunguza presha kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Oktoba 25.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Simba kumenyana na timu hiyo kutoka Guinea ya Ikweta lakini kwa Barker haitakuwa mara ya kwanza.

Msimu uliopita Barker akiwa kocha wa Stellenbosch aliiongoza timu hiyo kuiondosha 15 de Agosto katika hatua kama hii kwenye kombe la Shirikisho kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1.

Stellenbosch walishinda mabao 4-1 katika mchezo wa kwanza nyumbani na kulazimishwa suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa pili ugenini.

Licha ya kutoifahamu vyema klabu hiyo kwa kuwa hawana taarifa za kutosha, Barker amesema anao mwanga wa aina ya timu wanakwenda kukutana nayo.

“Siku zote unapokuwa umeshacheza na timu, inakuwa rahisi kidogo kwa sababu unakuwa na picha ya aina ya timu unayokutana nayo. Unakuwa na uelewa wa namna inavyocheza na changamoto unazoweza kukutana nazo, jambo linalokusaidia katika maandalizi.

“Lakini kila msimu una changamoto mpya na wao pia wamebadilisha baadhi ya wachezaji, hivyo huwezi kutegemea uzoefu huo pekee”

“Tunaiheshimu 15 de Agosto na tunajua kwamba ili kupata matokeo tunayoyahitaji, lazima tuingie uwanjani tukiwa tumejiandaa vizuri kimwili na kiakili, huku tukitekeleza mpango wetu wa mchezo ambao tumekuwa tukiufanyia kazi katika maandalizi,” alisema

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
2h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
6h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
20h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
1d ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 18 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 18 2026
2d ago
READ MORE β†’