FT : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL R1

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1h ago
FT : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL R1

Ilikuwa ni Doumbia Day! Ndivyo unavyoweza kusema baada kusubiri kwa muda mrefu hatimaye mashabiki wa Simba leo wamemshuhudia mshambuliaji wao pendwa Ibrahim Doumbia akifungua akaunti ya mabao.

Ni katika ushindi wa mabao 6-1 ambao Simba wameupata dhidi ya 15 de Agosto kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa (CAFCL).

Kama ilivyo kawaida yao, vijana wa kocha Steve Barker walitawala mchezo huo na licha ya kufunga bao moja tu hadi mapumziko, ilikuwa ni suala la muda tu kwa 15 de Agosto kubebeshwa kapu la mabao.

Nathaniel Chilambo ndiye aliyefungua kalamu ya mabao mwishoni mwa kipindi cha kwanza akitumia makosa ya safu ya ulinzi ya 15 de AGosto.

Kipindi cha pili ndio balaa likawakumba 15 de Agosto wakishindwa kuhimili kasi ya Wana lunyasi ambao ni wazi kwa sasa wako katika kiwango bora wakionyesha dalili za kuwa na msimu wa mafanikio makubwa kwenye ligi ya mabingwa.

Lakini subira ya Wanasimba kwa Doumbia aliyeingia kipindi cha pili ikalipwa kwa staili ya aina yake, mshambuliaji huyo kutoka Mali akiweka kambani mabao mawili.

Bao la kwanza aliweza kumtoka mlinzi wa mwisho pamoja na mlinda lango kabla ya kufunga la pili akimalizia krosi ya Makgalwa ambaye pia alifunga bao moja kwenye mchezo huo.

Mabao mengine ya Simba yalifungwa na Elie Mpanzu na Anicet Oura huku de Agosto wakipata bao la kufutia machozi dakika za lala salama.

Unaweza kusema Simba tayari imetinga makundi baada ya ushindi huo wa kibabe kwani ili kufuzu de Agosto watahitaji kushinda 5-0 mchezo wa marudiano!

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Goals : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL (FT)
Goals : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL (FT)
16m ago
READ MORE β†’
Kikosi : 15 de Agosto vs Simba, CAFCL R1
Kikosi : 15 de Agosto vs Simba, CAFCL R1
4h ago
READ MORE β†’
BIG SCREEN iko Mwembeyanga
BIG SCREEN iko Mwembeyanga
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; 15 de Agosto vs Simba, CAFCL R1
Matchday; 15 de Agosto vs Simba, CAFCL R1
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 21 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 21 2026
11h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili 15 de Agosto yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili 15 de Agosto yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
15 de Agosti waruhusu mashabiki
15 de Agosti waruhusu mashabiki
1d ago
READ MORE β†’
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1d ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
1d ago
READ MORE β†’