Kisa mashabiki: Simba yatozwa faini ya Sh Milioni 15

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1h ago
Kisa mashabiki: Simba yatozwa faini ya Sh Milioni 15

Klabu ya Simba SC imekumbana na faini ya jumla ya Sh milioni 15 kutoka Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), kufuatia makosa yaliyofanywa na mashabiki wake katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC.

Mchezo huo wa dabi ya Kariakoo ulipigwa Oktoba 10, 2026, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, huku matukio ya utovu wa nidhamu yaliyohusisha baadhi ya mashabiki wa Simba yakisababisha klabu hiyo kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Sh Milioni 10 kwa kurusha chupa

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Simba imetozwa faini ya Sh milioni 10 kutokana na mashabiki wake kurusha chupa uwanjani zaidi ya mara moja wakati wa mchezo huo.

Bodi hiyo imeeleza kuwa kosa hilo limejirudia katika msimu wa 2026/2027, baada ya mashabiki wa klabu hiyo kufanya kitendo kama hicho katika mchezo mwingine dhidi ya Pamba Jiji.

Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 48:1 ya Ligi Kuu inayohusu udhibiti kwa klabu, hatua inayolenga kuimarisha nidhamu na kuhakikisha usalama wakati wa michezo ya ligi.

Sh Milioni 5 kwa kuingia eneo la kuchezea

Mbali na faini ya kurusha chupa, Simba pia imepigwa faini ya Sh milioni 5 baada ya mashabiki wake kuvamia eneo la kuchezea wakati mchezo dhidi ya Yanga ukiendelea.

Katika tukio hilo, mmoja wa mashabiki aliripotiwa kumfuata kijana aliyekuwa akikusanya mipira nje ya uwanja wa kuchezea na kumfanyia fujo kabla ya kudhibitiwa na walinzi wa uwanja.

Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo huo ambao Wekundu wa Msimbazi walionyesha kandanda safi wakifunga mabao yao kipindi cha pili kupitia kwa Neo Maema na Elie Mpanzu.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 23 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 23 2026
4h ago
READ MORE β†’
Simba yajivunia rekodi ya kibabe CAFCL
Simba yajivunia rekodi ya kibabe CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza viingilio vya mchezo wa marudiano dhidi ya 15 de Agosto
Simba yatangaza viingilio vya mchezo wa marudiano dhidi ya 15 de Agosto
19h ago
READ MORE β†’
Doumbia atakuwa bora zaidi - Barker
Doumbia atakuwa bora zaidi - Barker
1d ago
READ MORE β†’
Chilambo labda nafasi ya kipa tu ndio hachezi
Chilambo labda nafasi ya kipa tu ndio hachezi
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL (FT)
Highlights : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 22 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 22 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL R1
FT : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL R1
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : 15 de Agosto vs Simba, CAFCL R1
Kikosi : 15 de Agosto vs Simba, CAFCL R1
1d ago
READ MORE β†’
BIG SCREEN iko Mwembeyanga
BIG SCREEN iko Mwembeyanga
1d ago
READ MORE β†’