Simba uhakika Pot 2 makundi CAFCL

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3h ago
Simba uhakika Pot 2 makundi CAFCL

Huku ikiwa imebakiza hatua moja tu ya kukamilisha ratiba ili kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), klabu ya Simba SC inatarajiwa kuwa Poti 2 kwenye droo ya makundi inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo nchini Misri.

Wekundu wa Msimbazi wanaingia kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya 15 de Agosto ya Guinea ya Ikweta Jumapili hii, Oktoba 25, 2026, wakiwa na mtaji mnono wa ushindi wa mabao 6-1 walioupata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es Salaam.

Mabao kutoka kwa Ibrahim Doumbia, Nathaniel Chilambo, Elie Mpanzu, Keletso Makgalwa na Anicet Oura yaliwapa Simba uhakika wa asilimia 99 kutinga hatua ya makundi, jambo linalofanya mchezo wa Jumapili kuwa wa kukamilisha ratiba na kutoa burudani kwa mashabiki.

Habari njema zaidi kwa mashabiki wa Simba ni kuwa nafasi ya Simba kwenye viwango vya ubora vya CAF vya miaka mitano (CAF 5-Year Ranking) inawabeba moja kwa moja hadi Poti la Pili.

Hatua hii inamaanisha Simba itakutana na kigogo mmoja tu kutoka poti 1 itakayokuwa na timu kama Mamelodi Sundowns, RS Berkane, Esperance na Zamalek kama zote zitafuzu makundi.

Katika poti 2 Simba huenda ikaungana na watani zao Yanga, Pyramids na Al Hilal. Wakati Yanga ikiwa tayari imefuzu, Simba, Pyramids na Al Hilal zote zinatarajiwa kufuzu baada ya kushinda mechi zao za kwanza.

Vigogo wengine hatarini

Wakati Simba ikiwa na uhakika wa asilimia 99, hali ni tofauti kwa miamba mingine ya Afrika inayopambana wikendi hii kukwepa mishale ya kuondolewa mashindanoni. Esperance de Tunis ya Tunisia ipo hatarini baada ya kupoteza 0-1 mchezo wa kwanza dhidi ya Asswehly SC ya Libya, huku Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ikilazimika kushinda nyumbani baada ya suluhu ya 0-0 ugenini dhidi ya Wiliete SC.

Droo kamili ya makundi inatarajiwa kuchezwa jijini Cairo, Jumatano ya tarehe 28 Oktoba 2026.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Doumbia awashukuru mashabiki wa Simba kwa uvumilivu, asema kazi ndiyo imeanza
Doumbia awashukuru mashabiki wa Simba kwa uvumilivu, asema kazi ndiyo imeanza
11h ago
READ MORE β†’
Kisa mashabiki: Simba yatozwa faini ya Sh Milioni 15
Kisa mashabiki: Simba yatozwa faini ya Sh Milioni 15
14h ago
READ MORE β†’
Simba yajivunia rekodi ya kibabe CAFCL
Simba yajivunia rekodi ya kibabe CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 23 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 23 2026
17h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza viingilio vya mchezo wa marudiano dhidi ya 15 de Agosto
Simba yatangaza viingilio vya mchezo wa marudiano dhidi ya 15 de Agosto
1d ago
READ MORE β†’
Doumbia atakuwa bora zaidi - Barker
Doumbia atakuwa bora zaidi - Barker
1d ago
READ MORE β†’
Chilambo labda nafasi ya kipa tu ndio hachezi
Chilambo labda nafasi ya kipa tu ndio hachezi
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL (FT)
Highlights : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 22 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 22 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL R1
FT : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL R1
2d ago
READ MORE β†’