Simba imetinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL) kibabe baada ya kuifumua 15 de Agosto mabao 3-0 katika mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya michuano hiyo.
Ilikuwa ni shoo ya dakika 45 za kipindi cha pili iliyosimamiwa na Elie Mpanzu, Anicet Oura na Keletso Makgalwa waliofunga mabao ya Wekundu hao wa Msimbazi.
Baada ya kung'ara kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza, mambo hawakuwa mazuri kwa mshambuliaji Ibrahim Doumbia ambaye unaweza kusema kipindi cha kwanza alichelewesha ushindi wa Simba akikosa nafasi za wazi.
Simba imetnga makundi kwa ushindi wa jumla wa mabao 9-1 na kuweka rekodi ya aina yake.
Hii ni mara ya sita kwa Simba kutinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa.

ADVERTISE HERE