Wakati kikosi cha Simba kikiwa tayari kimewasili mkoani Arusha kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Fountain Gate, mtanage huo umesogezwa mbele kwa siku moja.
Awali mchezo huo ulipangwa kupigwa Jumatano Oktoba 28, sasa utapigwa Oktoba 29 katika uwanja wa Tanzante Kwaraa, Manyara.
Changamoto za usafiri kwa wenyeji Fountain Gate inatajwa kuwa sababu iliyopelekea mtanange huo kusogezwa mbele.
Fountain Gate walikuwa Shinyanga ambapo jana walimenyana na Geita Gold.
Simba iliondoka jijini Dar es salaam mapema leo ambapo tayari kikosi kiko mkoani Arusha kabla ya kuungansha kuelekea Manyara.
ADVERTISE HERE