Klabu ya soka ya Simba imetangaza rasmi kuwa Mkutano Mkuu wa Kawaida wa Mwaka 2026 pamoja na uchaguzi mkuu wa viongozi wapya utafanyika tarehe 3 Januari 2027 jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo inakuja baada ya mchakato wa kisheria kukamilika kufuatia kibali kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Michezo nchini.
Bodi ya Wakurugenzi ya Simba iliwasilisha ombi rasmi la kusogeza mbele mkutano huo mnamo tarehe 23 Septemba 2026. Kufuatia ombi hilo, tarehe 22 Oktoba 2026, Msajili alitoa idhini kwa klabu hiyo kufanya uchaguzi wake ndani ya kipindi cha siku 90, na hivyo kupelekea kupangwa kwa tarehe hiyo ya mapema mwezi Januari.
Uchaguzi huu unatarajiwa kuwa na umuhimu wa kipeke, wanachama na mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona safu mpya ya uongozi itakayochukua jahazi la kuongoza klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam.
Taarifa zaidi kuhusu ratiba ya kuchukua na kurudisha fomu za ugombea pamoja na nafasi zinazowaniwa zinatarajiwa kutangazwa hivi karibuni na kamati ya uchaguzi ya klabu.