Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10h ago
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL

Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, ameweka wazi msimamo wake kuelekea hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, akisisitiza kuwa kikosi chake hakina sababu ya kuiogopa timu yoyote, licha ya ukubwa wa wapinzani kitakaokutana nao.

Barker amesema kinachopewa kipaumbele kwa sasa si kujadili majina ya timu ambazo Simba inaweza kupangwa nazo, bali kujiandaa kukabiliana na changamoto yoyote itakayojitokeza katika hatua hiyo ya mashindano.

Kauli hiyo imekuja wakati Wekundu wa Msimbazi wakijiandaa kuingia kwenye vita ya makundi wakiwa na matumaini ya kusonga mbele na kutimiza lengo lao msimu huu.

Droo ya hatua ya makundi inatarajiwa kufanyika nchini Misri siku ya Jumatano, Oktoba 28

Simba ilijihakikishia nafasi katika hatua hiyo baada ya kuonyesha ubora dhidi ya 15 de Agosto ya Equatorial Guinea. Katika mchezo wa marudiano wa raundi ya pili, uliochezwa Jumapili iliyopita, timu hiyo ya Tanzania ilishinda mabao 3-0, na kufanya ushindi wa jumla kufikia mabao 9-1.

Akizungumzia maandalizi ya hatua inayofuata, Barker amesisitiza kuwa hakuna nafasi ya kuchagua wapinzani katika mashindano yenye ushindani mkubwa kama Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hakuna timu nyepesi. Ili kufanya vizuri, unatakiwa kuwa tayari kupangwa au kukutana na timu yoyote,” amesema Barker.

Barker amesema kufuzu hatua ya makundi ilikuwa sehemu ya malengo ya awali yaliyokuwa yamewekwa, lakini safari bado haijakamilika. Sasa macho yanaelekezwa kwenye droo itakayoamua wapinzani wa Simba na changamoto zitakazowakabili katika kundi lao.

“Moja ya hesabu zetu za mwanzo ilikuwa kufika hatua ya makundi, jambo ambalo tumelifanikisha kwa kishindo. Sasa ni wakati wa kusubiri kundi tutakalopangwa,” amesema.

Hata hivyo, kocha huyo amesisitiza kuwa Simba haitakiwi kukimbilia kufanya hesabu za hatua za mbali bila kwanza kutekeleza majukumu yake katika hatua inayofuata.

Lengo lililowekwa ni kufika robo fainali, lakini Barker anaamini safari ya kulifikia inahitaji maandalizi, umakini na uwezo wa kupambana katika kila mchezo.

“Tunapigania nafasi ya kwenda robo fainali. Ni muhimu kupambana hatua kwa hatua, baada ya hapo ndipo tutakuwa na hesabu nyingine zaidi,” amesema Barker.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
11h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’