Meneja wa habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema wamepania kumaliza hasira dhidi ya Fountain Gate kwenye mchezo wa ligi kuu utakaopigwa kesho Alhamisi kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa huko Manyara.
Simba inarudi tena Tanzanite Kwaraa katika uwanja ambao Mnyama hana kumbukumbu nzuri nao mara ya mwisho akilazimishwa sare ya bao 1-1.
Ahmed amesema wakati huu ni Simba tofauti inayokwenda kucheza kwenye uwanja huo hivyo matarajio ya kuibuka na ushindi ni makubwa.
"TUnafahamu kwamba kwenye uwanja huu wa Tanzanite Kwaraa hatujawahi kupata ushindi lakini hii ni Simba ya tofauti kabisa"
"Hii ni Simba mpya ambayo huwezi kucheza nayo dakika 90 bila kukudhuru. Ni Simba ambayo huwezi kushikilia bomba kwa dakika 90 usipelekewe pumzi ya moto"
"Ili waweze kupata sare na Simba maana yake itabidi wazuie kwelikweli sasa kumzuia Oura dakika 90, kumzuia Libasse dakika 90, kumzuia Chama dakika 90, mipango ikibadilika mwalimu anaweza kumuweka Keletso Makgalwa kumzuia dakika 90 itawezekana?"
"Labda kama Mwenye ez Mungu hajapanga tushinde mchezo huo lakini kwa ubora tuliokuwa nao, hakuna rekodi yoyote ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba," alisema Ahmed