Matchday ; Simba vs Namungo Fc, NBC PL, Nov 2

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3h ago
Matchday ; Simba vs Namungo Fc, NBC PL, Nov 2

Vinara wa ligi kuu ya NBC Simba SC, leo usiku watashuka katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, kuwakaribisha Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, huku wakisaka rekodi ya kusimamisha ushindi wa 10 mfululizo msimu huu.

Simba inaingia uwanjani ikiwa na morali ya juu baada ya kushinda michezo yote tisa ya kwanza ya msimu na kujizolea alama 27, hatua inayowafanya kuongoza ligi hiyo kwa kishindo.

Hata hivyo, kibarua hakitakuwa chepesi mbele ya Namungo FC, ambao kwa sasa wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 15 baada ya kucheza mechi 10.

Namungo wanaonekana kupania kuvuruga karamu ya ushindi ya Wekundu wa Msimbazi, hata hivyo watahitaji kuwa bora kwelikweli mbele ya Simba inayofunga kila timu inayokuja mbele yake.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 1:00 usiku katika dimba la Uhuru, uwanja ambao hakuna timu iliyotoka salama mbele ya Simba huku baadhi ya timu zikiondoka na kapu la mabao.

Namungo Fc walikuwa wa kwanza kubebeshwa zigo la mabao na SImba kwenye uwanja huo wakipigwa mabao 6-1 idadi ambayo pia 15 de Agosto walikumbana nayo kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa.

Je leo itakuwa zamu ya Namungo?

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kujichimbia Kenya mapumziko kalenda ya FIFA
Simba kujichimbia Kenya mapumziko kalenda ya FIFA
2h ago
READ MORE β†’
Mo aongeza mkwanja wa bonasi Simba
Mo aongeza mkwanja wa bonasi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 02 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 02 2026
6h ago
READ MORE β†’
Huu hapa uzi wa ligi ya mabingwa 2026/27
Huu hapa uzi wa ligi ya mabingwa 2026/27
15h ago
READ MORE β†’
Matola atahadharisha mechi dhidi ya Namungo Fc, mkakati ni alama tatu
Matola atahadharisha mechi dhidi ya Namungo Fc, mkakati ni alama tatu
20h ago
READ MORE β†’
TFF yaingilia kati uchaguzi SImba 'mchakato lazima uendelee'
TFF yaingilia kati uchaguzi SImba 'mchakato lazima uendelee'
20h ago
READ MORE β†’
Simba vs Namungo Fc; Ahmed awaalika mashabiki dimba la Uhuru
Simba vs Namungo Fc; Ahmed awaalika mashabiki dimba la Uhuru
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 01 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 01 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mligo, Chilambo wajumuishwa kikosi cha Stars
Mligo, Chilambo wajumuishwa kikosi cha Stars
1d ago
READ MORE β†’
Namungo Fc wanatafuta kipigo kizito kutoka kwa Simba
Namungo Fc wanatafuta kipigo kizito kutoka kwa Simba
1d ago
READ MORE β†’