Tutafanyia kazi mapungufu mapumziko ya FIFA - Barker

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1h ago
Tutafanyia kazi mapungufu mapumziko ya FIFA - Barker

Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker amewapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa kupambana kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo ambao Simba ilihitaji dakika 11 za mwishoni kusawazisha na kufunga bao la ushindi.

Barker amesema zipo changamoto ambazo wanahitaji kuzifanyia kazi wakati huu ambao ligi inasimama kupisha kalenda ya FIFA.

Barker ametaja changamoto hizo ni eneo la safu ya ulinzi na timu kupoteza umiliki wa mchezo hasa baada ya dakika 45.

"Naawapongeza wachezaji wangu, tulilazimika kupambana kupata ushindi huu, haikuwa mechi rahisi kwetu. Tunapaswa kufanyia kazi maeneo yaliyoonyesha mapungufu"

"Mapumziko ya ligi yamekuja wakati sahihi kwani tuna nafasi ya kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza katika michezo ya hivi karibuni, hasa kushindwa kudhibiti mchezo na makosa ya kiulinzi"

"Tumekuwa tukianza vizuri michezo lakini tunapoteza mwelekeo baada ya dakika 30 hadi 45, hali inayowapa wapinzani nafasi ya kurejea mchezoni. Lazima tuboreshe umiliki wa mpira na uimara wa safu ya ulinzi kabla ya michezo ijayo," alisema Barker

Katika mchezo dhidi ya Namungo Fc, kukosekana kwa beki Ismail Toure ilionekana dhahiri kuipa changamoto Simba kwenye safu ya ulinzi Barker akimuanzisha beki kinda Ibrahim Nindi.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Ni rekodi ushindi mechi 20 mfululizo Ligi Kuu - Magori
Ni rekodi ushindi mechi 20 mfululizo Ligi Kuu - Magori
1h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-2 Namungo Fc, NBC PL (FT)
Highlights; Simba 3-2 Namungo Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 03 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 03 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-2 Namungo Fc, NBC PL
FT : Simba 3-2 Namungo Fc, NBC PL
12h ago
READ MORE β†’
Goals; Simba 3-2 Namungo Fc, NBC PL (FT)
Goals; Simba 3-2 Namungo Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs Namungo Fc, NBC PL, Nov 2
Kikosi : Simba vs Namungo Fc, NBC PL, Nov 2
15h ago
READ MORE β†’
Simba kujichimbia Kenya mapumziko kalenda ya FIFA
Simba kujichimbia Kenya mapumziko kalenda ya FIFA
22h ago
READ MORE β†’
Mo aongeza mkwanja wa bonasi Simba
Mo aongeza mkwanja wa bonasi Simba
22h ago
READ MORE β†’
Matchday ; Simba vs Namungo Fc, NBC PL, Nov 2
Matchday ; Simba vs Namungo Fc, NBC PL, Nov 2
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 02 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 02 2026
1d ago
READ MORE β†’