Doumbia ajumuishwa timu ya Taifa ya Mali

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2h ago
Doumbia ajumuishwa timu ya Taifa ya Mali

Mshambuliaji wa klabu ya Simba SC, Ibrahim Doumbia, amejumuishwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Mali kitakachoshuka uwanjani mwezi huu Novemba kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027.

Hii ni mara ya kwanza kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kuitwa kwenye kikosi cha wakubwa cha Mali cha 'The Eagles', ikiwa ni matokeo ya kiwango chake bora anachoendelea kukionyesha tangu ajiunge na Wekundu wa Msimbazi mwezi Julai mwaka huu.

Kocha Mkuu wa Mali, Anthony da Silva, ametangaza kikosi cha wachezaji 25 watakaovaana na Rwanda katika mechi mbili za kalenda ya FIFA (nyumbani na ugenini) zitakazopigwa kati ya Novemba 13 na Novemba 17, 2026.

Wito huo wa Doumbia unaongeza idadi ya wachezaji wanaoiwakilisha Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBCL) nchini Mali, kwani atakuwa sambamba na mlinda wa Yanga, Djigui Diarra, ambaye pia amejumuishwa kwenye orodha ya makipa watatu wa kikosi hicho.

Kwenye safu ya ushambuliaji, Doumbia anatarajiwa kupigania namba na wachezaji wengine wa kimataifa wa Mali wanaokipiga barani Ulaya, wakiwemo Lassine Sinayoko (Paris FC), Dorgeles Nene (Fenerbahce), na Gaoussou Diarra (Feyenoord).

Doumbia alijiunga na Simba SC akitokea klabu ya AS Korofina ya Mali ambako alimaliza msimu kama mfungaji bora wa ligi hiyo, na kuitwa kwake kwenye kikosi cha wakubwa kunathibitisha thamani yake.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Doumbia, Keletso, Morice ni silaha za siri za Barker
Doumbia, Keletso, Morice ni silaha za siri za Barker
5h ago
READ MORE β†’
Toure ndio Waziri wa ulinzi pale Msimbazi
Toure ndio Waziri wa ulinzi pale Msimbazi
8h ago
READ MORE β†’
Simba yaomba kutumia uwanja wa New Amaan Complex makundi CAFCL
Simba yaomba kutumia uwanja wa New Amaan Complex makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 04 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 04 2026
11h ago
READ MORE β†’
Simba yaalikwa kumbukumbu ya Odinga Kenya
Simba yaalikwa kumbukumbu ya Odinga Kenya
1d ago
READ MORE β†’
Tutafanyia kazi mapungufu mapumziko ya FIFA - Barker
Tutafanyia kazi mapungufu mapumziko ya FIFA - Barker
1d ago
READ MORE β†’
Ni rekodi ushindi mechi 20 mfululizo Ligi Kuu - Magori
Ni rekodi ushindi mechi 20 mfululizo Ligi Kuu - Magori
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-2 Namungo Fc, NBC PL (FT)
Highlights; Simba 3-2 Namungo Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 03 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 03 2026
1d ago
READ MORE β†’
Goals; Simba 3-2 Namungo Fc, NBC PL (FT)
Goals; Simba 3-2 Namungo Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’