Ratiba ya Simba kufunga mwaka 2026

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1h ago
Ratiba ya Simba kufunga mwaka 2026

Baada ya kusimama kwa Ligi Kuu ya NBC kupisha kalenda ya kimataifa ya FIFA, miamba ya soka nchini, klabu ya Simba SC, inatarajia kurejea uwanjani kwa kishindo kupambana na ratiba ngumu ya kuhitimisha mwaka 2026.

Wekundu wa Msimbazi watakuwa na kibarua kizito cha kusaka alama tatu muhimu katika Ligi Kuu ya NBC, sambamba na kupeperusha bendera ya taifa katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).

Ratiba hiyo inaonyesha kuwa Simba itaanza kampeni yake Novemba 21, 2026, kwa kumenyana na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo jijini Dar es Salaam.

Baada ya mchezo huo, miamba hiyo itahamishia nguvu zake kwenye michuano ya CAFCL, ambapo kati ya Novemba 27 na 29, 2026, watakuwa wenyeji wa Orlando Pirates kutoka Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya CAF.

Mwezi Desemba utakuwa wa pilika nyingi zaidi kwa Simba. Mapema mwezi huo, kikosi hicho kitasafiri hadi ugenini kumenyana na Colombe FC katika mchezo mwingine wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kabla ya kurejea nchini kuivaa TRA United jijini Arusha mnamo Desemba 11.

Ratiba kamili ya Simba hadi kufikia mwisho wa mwaka huu wa 2026 itakuwa kama ifuatavyo:

  • Novemba 21, 2026: JKT Tanzania vs Simba SC (Uwanja wa JKT Isamuhyo – Ligi Kuu)
  • Novemba 27–29, 2026: Simba SC vs Orlando Pirates (Uwanja wa Nyumbani – Ligi ya Mabingwa Afrika)
  • Desemba 4–6, 2026: Colombe vs Simba SC (Ugenini – Ligi ya Mabingwa Afrika)
  • Disemba 4-8 2026 : Simba vs Dodoma Jiji (nyumbani - Ligi Kuu)
  • Desemba 11, 2026: TRA United vs Simba SC (Uwanja wa Sheikh Amri Abeid – Ligi Kuu)
  • Desemba 18–20, 2026: RS Berkane vs Simba SC (Ugenini – Ligi ya Mabingwa Afrika)
  • Desemba 31, 2026: Polisi Tanzania vs Simba SC (Uwanja wa Sheikh Amri Abeid – Ligi Kuu)

Simba imejipanga kufanya vyema kwenye mashindano yote, ikiwa na rekodi ya ushindi wa asilimia 100 mpaka sasa kwenye kila mechi waliyocheza msimu huu.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 06 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 06 2026
3h ago
READ MORE β†’
Nindi ana walimu wazuri Simba, atakuwa beki bora
Nindi ana walimu wazuri Simba, atakuwa beki bora
18h ago
READ MORE β†’
Barker, Mpanzu watwaa tuzo za ligi kuu Oktoba 2026
Barker, Mpanzu watwaa tuzo za ligi kuu Oktoba 2026
1d ago
READ MORE β†’
Wachezaji Simba wapewa mapumziko, kurejea Novemba 09
Wachezaji Simba wapewa mapumziko, kurejea Novemba 09
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi Novemba 05 2026
Magazeti ya leo Alhamisi Novemba 05 2026
1d ago
READ MORE β†’
Doumbia ajumuishwa timu ya Taifa ya Mali
Doumbia ajumuishwa timu ya Taifa ya Mali
1d ago
READ MORE β†’
Doumbia, Keletso, Morice ni silaha za siri za Barker
Doumbia, Keletso, Morice ni silaha za siri za Barker
1d ago
READ MORE β†’
Toure ndio Waziri wa ulinzi pale Msimbazi
Toure ndio Waziri wa ulinzi pale Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaomba kutumia uwanja wa New Amaan Complex makundi CAFCL
Simba yaomba kutumia uwanja wa New Amaan Complex makundi CAFCL
2d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 04 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 04 2026
2d ago
READ MORE β†’