Simba kurudi Uhuru CAFCL, ni baada ya CAF kuidhinisha

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
31m ago
Simba kurudi Uhuru CAFCL, ni baada ya CAF kuidhinisha

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeipa neema kubwa klabu ya Simba SC baada ya kuidhinisha rasmi Uwanja wa Uhuru uliopo jijini Dar es Salaam kutumika kwa ajili ya michezo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu wa 2026/2027.

Maamuzi hayo yamekuja kama muarobaini kwa miamba hiyo ya Msimbazi, ambayo sasa imepata kibali cha kuutumia uwanja huo kama ngome yao kuu ya nyumbani kufuatia kufungwa kwa Uwanja wa Benjamin Mkapa unaofanyiwa maboresho makubwa kuelekea fainali za AFCON 2027.

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, amethibitisha kupokelewa kwa barua hiyo ya idhini kutoka CAF, akibainisha kuwa ukaguzi wa mwisho uliridhishwa na maboresho ya miundombinu yaliyofanyika kwa ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa soka.

Kabla ya uwanja wa Uhuru kuidhinishwa, Simba ilichagua kutumia uwanja wa New Amaan Complex wa visiwani Zanzibar ambao ulikuwa uwanja pekee uliokuwa umekidhi vigezo vya CAF.

Simba SC, ambayo imepangwa katika Kundi C, itaanza kutumia rasmi uwanja huo wenye uwezo wa kubeba mashabiki 19,000 katika mchezo wao wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini, uliopangwa kuchezwa kati ya Novemba 27 na 29, 2026.

Ratiba inaonyesha pia Uhuru utawaalika RS Berkane ya Morocco mapema mwezi Januari 2027 kabla ya kumalizana na Colombe Sportive ya Cameroon.

Aidha klabu ya Singida BS nayo imechagua kutumia uwanja huo kwenye hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho (CAFCC)

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 07 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 07 2026
1h ago
READ MORE β†’
TFF yaweka hadharani ratiba ya uchaguzi Simba
TFF yaweka hadharani ratiba ya uchaguzi Simba
15h ago
READ MORE β†’
Hapo kwenye asisti Gueye ameshindikana
Hapo kwenye asisti Gueye ameshindikana
19h ago
READ MORE β†’
Kuna rekodi ya maisha Barker anaiweka Msimbazi
Kuna rekodi ya maisha Barker anaiweka Msimbazi
21h ago
READ MORE β†’
Ratiba ya Simba kufunga mwaka 2026
Ratiba ya Simba kufunga mwaka 2026
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 06 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 06 2026
1d ago
READ MORE β†’
Nindi ana walimu wazuri Simba, atakuwa beki bora
Nindi ana walimu wazuri Simba, atakuwa beki bora
1d ago
READ MORE β†’
Barker, Mpanzu watwaa tuzo za ligi kuu Oktoba 2026
Barker, Mpanzu watwaa tuzo za ligi kuu Oktoba 2026
1d ago
READ MORE β†’
Wachezaji Simba wapewa mapumziko, kurejea Novemba 09
Wachezaji Simba wapewa mapumziko, kurejea Novemba 09
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi Novemba 05 2026
Magazeti ya leo Alhamisi Novemba 05 2026
2d ago
READ MORE β†’