Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14h ago
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA

Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa kesho Jumamosi, Novemba 21 katika uwanja wa Isamuhyo, Mbweni.

Akizungumzia maandalizi kuelekea mchezo huo, Barker amesema ametumia vyema mapumziko ya kalenda ya FIFA akiamini vijana wake wako tayari kuendeleza wimbi la ushindi.

Hata hivyo Barker amesema anatambua JKT Tanzania ni timu ngumu hivyo watachukua tahadhari ili kuhakikisha wanapata ushindi.

"Maandalizi yanakwenda vizuri na tulianza kufanya hivyo wakati wa kalenda ya FIFA. Tunahitaji kuingia kwenye mchezo huu na umakini mkubwa."

"Lengo letu ni kupata ushindi ili kuendeleza matokeo mazuri tuliyokuwa nayo kabla ya mapumziko ya ligi," alisema Barker.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, kiungo Hussein Semfuko amesema kila mechi kwao ni muhimu na wanakwenda kupambania alama tatu.

"Wachezaji tumejipanga vizuri kwa ajili ya kuzipambania pointi tatu. Kila mechi kwetu ni muhimu kupata pointi tatu licha ya ugumu wa mpinzani."

"Tunahitaji kushinda ili kuhakikisha msimu huu tunatimiza malengo ya kutwaa ubingwa," alisema Semfuko

Simba SC Stories

Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
9h ago
READ MORE β†’
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
17h ago
READ MORE β†’
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
17h ago
READ MORE β†’
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
22h ago
READ MORE β†’
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
1d ago
READ MORE β†’
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Novemba 19 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Novemba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’