FT : JKT Tanzania 1-2 Simba, NBC PL, Nov 21

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1h ago
FT : JKT Tanzania 1-2 Simba, NBC PL, Nov 21

Simba imeendeleza ushindi kwa asilimia 100 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo mgumu uliopigwa uwanja wa Isamuhyo, Bweni.

Ushirikiano wa Libasse Gueye na Elie Mpanzu ndio ulioihakikishia Simba ushindi huo wawili hao wakifunga na kupeana asisti.

Baada ya JKT Tanzania kutangulia mapema dakika ya 10, Elie Mpanzu aliirejesha Simba mchezoni dakika ya 20 akimalizia kazi nzuri ya Gueye.

Dakika ya 34 Libasse Gueye akafunga bao la pili akimalizia kazi nzuri ya Mpanzu.

Kipindi cha pili Simba ilicheza kwa tahadhari kubwa huku JKT Tanzania wakimiliki mchezo kwa muda mwingi.

Hata hivyo uimara wa safu ya ulinzi ya Simba ikiongozwa na Rushine de Reuck ilikuwa imara kuhakikisha alama tatu zinapatikana licha ya mfululizo wa mashambulizi kutoka kwa JKT Tanzania dakika za lala salama.

Mnyama sasa amerejesha gap la alama tano kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 33.

Ni ushindi wa 11 mfululizo kwenye ligi! Hii ni rekodi ambayo inaweza kuishi kwa miaka mingi ijayo..!

Simba SC Stories

Highlights : JKT Tanzania 1-2 Simba, NBC PL (FT)
Highlights : JKT Tanzania 1-2 Simba, NBC PL (FT)
54m ago
READ MORE β†’
Kikosi : JKT Tanzania vs Simba, NBC PL, Nov 21
Kikosi : JKT Tanzania vs Simba, NBC PL, Nov 21
4h ago
READ MORE β†’
Orodha ya wagombea waliochukua fomu Simba
Orodha ya wagombea waliochukua fomu Simba
8h ago
READ MORE β†’
Simba ugenini dhidi ya JKT Tanzania leo, NBC PL
Simba ugenini dhidi ya JKT Tanzania leo, NBC PL
13h ago
READ MORE β†’
Chilambo ameumia kidole gumba, anaweza kufanyiwa upasuaji
Chilambo ameumia kidole gumba, anaweza kufanyiwa upasuaji
14h ago
READ MORE β†’
Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 21 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 21 2026
15h ago
READ MORE β†’
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
1d ago
READ MORE β†’
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
1d ago
READ MORE β†’
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
1d ago
READ MORE β†’