Libasse amtetea Doumbia, presha ni kubwa dhidi yake

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1d ago
Libasse amtetea Doumbia, presha ni kubwa dhidi yake

Kiungo mshambuliaji wa Simba Libasse Gueye amemtetea mchezaji mwenzake Ibrahim Doumbia kuwa anapaswa kupewa moyo na kuungwa mkono na mashabiki ili kumsaidia arejee kwenye ubora wake.

Gueye amesema kinachomsumbua Doumbia kwa sasa ni presha kubwa anayopewa nje ya uwanja ambayo kwa kiasi kikubwa inaathiri utendaji kazi wake.

"Doumbia ni mchezaji mzuri lakini changamoto kubwa inayomkabili ni presha ya nje ya uwanja."

"Amekuwa akishambuliwa sana, kila shabiki anasema lake hiki sio kitu kizuri. Kwa maoni yangu nadhani anapaswa kuungwa mkono na kuendelea kupewa moyo, atafanya vizuri."

"Wakati mwingine utamuona hana furaha kutokana na yale yanayoendelea dhidi yake nje ya uwanja hivyo nisema sio kitu kizuri, tumuunge mkono," alisema Libasse.

Doumbia amekuwa na vipindi tofauti tangu ajiunge na Simba, zipo nyakati amefanya vyema lakini zipo nyakati amehindwa kun'gara na hivyo kupelekea presha kubwa kutoka nje ya uwanja.

Tangu atue Msimbazi, Doumbia amepachika mabao mawili yote akiyafunga mechi za hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya 15 de Agosto ya Guinea ya Ikweta

Simba SC Stories

Deen amerejea kuendeleza alipoishia
Deen amerejea kuendeleza alipoishia
54m ago
READ MORE β†’
Pirates waanza safari kuifuata Simba
Pirates waanza safari kuifuata Simba
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 25 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 25 2026
5h ago
READ MORE β†’
Simba yaomba kuongezwa mashabiki Ligi ya Mabingwa
Simba yaomba kuongezwa mashabiki Ligi ya Mabingwa
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa siri ya Simba kushinda mechi mfululizo
Hii hapa siri ya Simba kushinda mechi mfululizo
19h ago
READ MORE β†’
Hatma ya wagombea wa nafasi za uongozi Simba kufahamika Ijumaa
Hatma ya wagombea wa nafasi za uongozi Simba kufahamika Ijumaa
1d ago
READ MORE β†’
Simba kuweka hadharani viingilio vya mchezo dhidi ya Orlando Pirates Jumatano
Simba kuweka hadharani viingilio vya mchezo dhidi ya Orlando Pirates Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mawindo ya Orlando Pirates yameanza Mo Simba Arena
Mawindo ya Orlando Pirates yameanza Mo Simba Arena
1d ago
READ MORE β†’
Tuko tayari kukabiliana na yeyote CAFCL - Maema
Tuko tayari kukabiliana na yeyote CAFCL - Maema
1d ago
READ MORE β†’