Simba yaomba kuongezwa mashabiki Ligi ya Mabingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3h ago
Simba yaomba kuongezwa mashabiki Ligi ya Mabingwa

Uongozi wa klabu ya Simba umeomba kwa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kuongezwa idadi ya mashabiki watakaoingia uwanja wa Uhuru kushuhudia mechi za nyumbani za Wekundu hao wa Msimbazi.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amethibitisha kuwa Simba imeomba kuruhusiwa kuingiza mashabiki 15,000 kuanzia mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Orlando Pirates utakaopigwa Jumapili, Novemba 29 uwanja wa Uhuru.

Ahmed amesema moja ya sababu zilizopelekea kuchelewa kutangaza viingilio vya mchezo huo ni kusubiri majibu ya maombi yao.

"Bado kuna matumaini ya kuruhusiwa mashabiki 15 kwenye dimba la Uhuru katika mechi zetu za nyumbani Ligi ya Mabingwa Afrika, kuanzia mchezo dhidi ya Orlando Pirates, Novemba 29."

"Tunasubiri majibu ya mwisho kutoka CAF, na hiyo ndiyo sababu tumechelewa kutangaza tiketi pamoja na hamasa," alisema Ahmed

Ahmed amebainisha kuwa mara watakapopata majibu Jumatano wiki hii, wataanza hamasa ambazo zitazinduliwa rasmi katika tawi la ‘Wekundu wa Jangwani’.

Simba SC Stories

Hii hapa siri ya Simba kushinda mechi mfululizo
Hii hapa siri ya Simba kushinda mechi mfululizo
3h ago
READ MORE β†’
Libasse amtetea Doumbia, presha ni kubwa dhidi yake
Libasse amtetea Doumbia, presha ni kubwa dhidi yake
9h ago
READ MORE β†’
Hatma ya wagombea wa nafasi za uongozi Simba kufahamika Ijumaa
Hatma ya wagombea wa nafasi za uongozi Simba kufahamika Ijumaa
9h ago
READ MORE β†’
Simba kuweka hadharani viingilio vya mchezo dhidi ya Orlando Pirates Jumatano
Simba kuweka hadharani viingilio vya mchezo dhidi ya Orlando Pirates Jumatano
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mawindo ya Orlando Pirates yameanza Mo Simba Arena
Mawindo ya Orlando Pirates yameanza Mo Simba Arena
1d ago
READ MORE β†’
Tuko tayari kukabiliana na yeyote CAFCL - Maema
Tuko tayari kukabiliana na yeyote CAFCL - Maema
1d ago
READ MORE β†’
Barker kuongea dozi Simba kukabiliana na ushindani unoongezeka
Barker kuongea dozi Simba kukabiliana na ushindani unoongezeka
1d ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse Gueye ni namba ya kutisha!
Huyu Libasse Gueye ni namba ya kutisha!
1d ago
READ MORE β†’
Simba vs Orlando Pirates ni Jumapili CAFCL
Simba vs Orlando Pirates ni Jumapili CAFCL
1d ago
READ MORE β†’