Transfer

Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi, Februari 04 2023

Joel JJ By Joel JJ
4 Feb 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi, Februari 04 2023

Manchester United na Paris St-Germain zinapaswa kulipa ada ya uhamisho ya angalau £90m ikiwa zinataka kumsajili mshambuliaji mahiri wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 24, katika dirisha la msimu wa joto. (ESPN)

Arsenal wameweka kipaumbele cha kukubaliana kandarasi mpya na nyota wake Bukayo Saka, 21, na beki wa Ufaransa William Saliba, 21, huku Manchester City ikimtaka winga huyo wa Uingereza. (Sports)

Baada ya dirisha dogo la usajili Chelsea wameelekeza nguvu zao katika kuongeza mkataba wa Mason Mount, 24. Mkataba wa sasa kiungo huyo wa kati wa England unamalizika msimu wa joto wa 2024. (90min)

Vyanzo vya karibu na mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang vinasema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ameshtushwa na amesikitishwa kuachwa nje ya kikosi cha Chelsea cha Ligi ya Mabingwa Ulaya na anaamini klabu hiyo inataka kumuondoa. (Telegraph)

Manchester United wamekubali kuongeza mkataba wa miaka minne wa winga mwenye umri wa miaka 18 Alejandro Garnacho, ambaye amekuwa akifanya vizuri na kucheza timu za taifa za vijana za Argentina. (AS kwa Kihispania)

Wafanyikazi wa Old Trafford wamegawanyika kuhusu iwapo mshambuliaji wa England Mason Greenwood mwenye umri wa miaka 21 aruhusiwe kuendelea na soka lake katika klabu hiyo ama la. (Guardian)

Greenwood anatazamia kuhamia China ili kuanza tena soka yake ikiwa United itaamua kumfuta kazi mara tu watakapokamilisha mchakato wao wa ndani. (Sun)

West Ham United na Everton watalazimika kusubiri hadi msimu wa joto kumsajili winga wa Suriname Sheraldo Becker baada ya Union Berlin kusita kumruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kuondoka mwezi Januari kwa sababu ya malengo yao ya Ligi ya Mabingwa. (Caught Offside)

Uhamisho wa beki wa kulia wa LA Galaxy Julian Araujo kwenda Barcelona umeshindikana baada ya Fifa kuamua kwamba nyaraka za kukamilisha uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ziliwasilishwa kwa kuchelewa mno. (ESPN)

Kiungo wa kati wa zamani wa Utrecht wa Marekani chini ya umri wa miaka 19 Taylor Booth, 21, anafuatiliwa na meneja wa Manchester United Erik ten Hag. (Mail)

BBC

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
1h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
1h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
2h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
2h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
2h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
2h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
3h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
4h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
15h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
15h ago
READ MORE →