Yanga - Namungo

Yanga vs Namungo Fc kinapigwa kwa Mkapa leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 Feb 2023
Yanga vs Namungo Fc kinapigwa kwa Mkapa leo

Vinara wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga leo watakuwa na nafasi ya kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi pale watakapoikabili Namungo Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Yanga itahitaji kushinda mchezo huo ili kurudisha gap la pointi dhidi ya watani zao Simba kuwa sita

Jana Simba ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Singida BS na hivyo kufikisha alama 53 wakati Yanga ikiwa kileleni na alama 56

Mchezo kati ya Yanga dhidi ya Namungo Fc haujawahi kuwa mwepesi, pamoja na Yanga kushinda mechi mbili za mwisho zilizokutanisha timu hizo

Katika misimu mitatu iliyopita, Yanga imeshinda mara mbili tu dhidi ya Namungo katika ligi kuu

Hivyo utakuwa mchezo mgumu ambao hakuna shaka utawapa burudani mashabiki wa soka nchini

Tangu ujio wa kocha Denis Kitambi, Namungo Fc wameimarika wakishika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 27

Pengine leo watahitaji kushinda mechi hiyo ngumu ili kuendelea kusogea nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi

Namungo Fc wametolewa kwenye michuano ya kombe la FA hivyo kama watahitaji kushiriki Kimataifa msimu ujao, basi wanahitaji kumaliza katika nafasi tatu za juu

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
1h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
4h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
5h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
5h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
6h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
7h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
8h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
8h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
21h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
21h ago
READ MORE β†’