Kesho Jumapili, Februari 05 klabu ya Simba itacheza mechi ya Kimataifa ya kirafiki dhidi ya Al Hilal ya Sudan
Al Hilal wako nchini katika kambi ya siku 10 kujiandaa na hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Tayari wamecheza mechi mbili dhidi ya Namungo Fc (1-1) na dhidi ya Azam Fc wakishinda 1-0
Simba imetangaza viingilio vya mchezo huo ambao utapigwa saa 10 jioni
