Transfer

Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Februari 06 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
6 Feb 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Februari 06 2023

Liverpool itasikiliza ofa msimu huu wa joto kwa beki wao wa kati wa zamani wa kimataifa wa Cameroon Joel Matip, 31, ambaye mkataba wake Anfield unamalizika mwaka 2024. (Football Insider)

Kocha mkuu wa West Brom Mhispania Carlos Corberan, 39, anawania kuchukua nafasi ya Jesse Marsch iwapo Leeds United itaamua kumtimua kocha huyo. (Mail)

Meneja wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho anataka 'kurejea' Stamford Bridge kwa kipindi cha tatu na Mreno huyo, 60, 'alijiweka karibu' wanunuzi wapya wakati klabu ilipoanza kuuzwa. (NipeMesport)

Chelsea pia wako tayari kumwajiri meneja wa zamani wa Hispania Luis Enrique, 52, kama mkufunzi mpya ikiwa watamtimu mkufunzi wa sasa Graham Potter. (Fichajes)

Barcelona wanafuatilia hali ya mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang katika klabu ya Chelsea huku wakipanga kumrejesha Camp Nou mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33. (Football transfers)

Newcastle United itaendelea kumfuatilia kiungo wa kati wa England Conor Gallagher, 22, baada ya kufanya mazungumzo na Chelsea kuhusu uhamisho wa Januari. (Football Insider)

Liverpool na Aston Villa zinaripotiwa kuwa tayari 'kuijaribu Athletic Bilbao katika dirisha la msimu ujao wa joto kwa kupeleka ofa kwa ajili ya winga wao wa Kihispania Nico Williams, 20, na kiungo wa kati wa Hispania Oihan Sancet, 22. (AS via Teamtalk).

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Hasan Salihamidzic amesema ada ya euro 70m (£62m) iliyowekwa katika mkataba wa mkopo wa beki wa pembeni wa Manchester City na Ureno Joao Cancelo, 28, itakuwa "ngumu" kwa klabu hiyo. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho, 30, anahusishwa kwa uhamisho wa mkopo kwenda Galatasaray baada ya msimu mgumu akiwa na Aston Villa. (Sun)

Mkurugenzi wa michezo wa Paris St-Germain Luis Campos amethibitisha kuwa klabu hiyo iko kwenye mazungumzo na mshindi wa Kombe la Dunia la Argentina Lionel Messi, 35, kuhusu kandarasi mpya. (Mail)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
3h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
3h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
4h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
7h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
11h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
11h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
12h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
12h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
13h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
14h ago
READ MORE β†’