Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeziruhusu klabu zinazoshiriki hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho kuruhusu mashabiki kuingia viwanjani katika mechi zao
Kulingana na taarifa iliyotolewa na CAF, hakuna kiwango elekezi kwa mashabiki kama ilivyokuwa kwa misimu miwili iliyopita
Ni baada ya Shirikisho hilo kujiridhisha nchi za barani Afrika zimefanikiwa katika udhibiti wa maambukizi ya virusi vya corona
Hii ni habari njema kwa klabu za Tanzania Simba na Yanga ambazo zinashiriki hatua ya makundi ya michuano hiyo
Simba inacheza ligi ya mabingwa ambapo mchezo wake wa kwanza nyumbani ni Februari 18 dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco wakati Yanga wanacheza kombe la Shirikisho mechi yao ya kwanza nyumbani ni dhidi ya TP Mazembe Februari 19