Transfer

Tetesi za soka Ulaya, Jumanne, Februari 07 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 Feb 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumanne, Februari 07 2023

Paris St-Germain wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva, 28, ambaye yuko tayari kuondoka Manchester City, lakini inaweza kukabiliana na ushindani kutoka kwa Barcelona. (Le10 Sport)

Manchester United itajaribu kuwauza mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 27, beki wa kati wa England Harry Maguire, 29, na beki wa kushoto wa Brazil Alex Telles, 30, katika msimu wa joto huku klabu hiyo ikilenga kutoa nafasi kwa mshambuliaji mpya kutoka klabu ya Tottenham nahodha wa Uingereza. Harry Kane 29, au mchezaji wa kimataifa wa Napoli mwenye umri wa miaka 24 Victor Osimhen.

Tottenham haitamuuza mfungaji bora wa klabu Kane kwa klabu pinzani msimu huu wa joto. (Times)

Manchester United itahitajika kulipa pauni milioni 120 kumnunua kiungo wa kati wa England Declan Rice, 24, kutoka West Ham, baada ya dau la pauni milioni 100 kukataliwa msimu uliopita. (TalkSport)

Carlos Corberan wa West Brom anaongoza kwenye orodha fupi ya Leeds ya kocha wa kuchukua nafasi ya Jesse Marsch aliyetimuliwa. (Guardian)

Real Madrid wanaamini kuwa kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 19, atachagua kuhamia ligi kuu England atakapoondoka Borussia Dortmund. (Athletic)

Wamiliki wa Southampton walijadili mustakabali wa meneja Nathan Jones baada ya timu hiyo kuchapwa 3-0 Jumamosi na Brentford lakini wanatazamiwa kuendelea kubaki naye kwa sasa. (Sport)

Jones anatarajiwa kuiongoza timu hiyo katika mechi ya nyumbani ya Southampton dhidi ya Wolves Jumamosi. (90Min)

Meneja wa zamani wa Southampton Ralph Hasenhuttl anaongoza mbio za kuwa meneja mpya wa klabu ya Ujerumani ya Hoffenheim baada ya klabu hiyo kumtimua Andre Breitenreiter. (Sky Sports)

Chelsea wanamfuatilia mlinda mlango wa Porto na Ureno Diogo Costa, 23, huku wakitarajia kushughulikia mustakabali wa mlinda mlango wao katika majira ya joto. (90Min)

Inter Milan wamemuongeza mlinzi wa Fulham Tosin Adarabioyo, 25, kwenye orodha ya nyota inayowasaka kuchukua nafasi ya mlinzi wa kati wa Slovakia Milan Skriniar, 27, ambaye anatarajiwa kuondoka katika kikosi hicho cha Serie A mkataba wake utakapokamilika msimu wa joto. (Tuttomercatoweb)

Kocha wa zamani wa Newcastle United, Steve Bruce, alikataa nafasi ya kuifundisha klabu yake ya zamani ya Wigan Athletic baada ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kumuomba achukua nafasi ya kocha Kolo Toure aliyetimuliwa hivi majuzi. (Football Insider)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
6h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
6h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
10h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
14h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
15h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
16h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
17h ago
READ MORE β†’