Al Ahly - Real Madrid

Al Ahly dhidi ya Real Madrid Club World Cup

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 Feb 2023
Al Ahly dhidi ya Real Madrid Club World Cup

Kesho Jumatano, Al Ahly itamenyana na mabingwa wa kihistoria wa Ligi Mabingwa Ulaya, Real Madrid kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia ngazi ya klabu

Bao la dakika za lala salama lililowekwa nyavuni na Mohamed Afsha dakika ya 88 wikiendi iliyopita limeipeleka Al Ahly nusu fainali katika michuano hiyo inayochezwa Morocco.

Al Ahly iliifunga bao 1-0 Seattle Sounders kwenye Uwanja wa Tangier, lakini ina kibarua dhidi ya Madrid yenye historia ya kubeba kombe hilo mara nne.

Madrid ilijikuta katika wakati mgumu na kukubali kichapo cha bao 1-0 kwenye mechi ya La Liga ilipomenyana dhidi ya Mallorca wikiendi iliyopita.

Baada ya kipigo hicho Madrid imeachwa pointi nane na Barcelona kwenye msimamo wa La Liga baada ya ushindi wake wa mabao 3-0 dhidi ya Sevilla.

Madrid imesuasua katika mechi zake za hivi karibuni lakini Kocha Carlo Ancelotti amedai kikosi chake kina majeruhi wengi.

Katika mechi nyingine ya robo fainali Al Hilal kutoka Saudia Arabia iliifunga Wydad Athletic kwa penalti 5-3, timu hiyo itacheza nusu fainali ya kwanza leo dhidi ya Flamengo.

Fainali ya Kombe la Dunia ngazi ya klabu itachezwa Februari 11 mwaka huu jijini Rabat, Morocco.

Madrid inashiriki michuano hii mara sita 2014, 2016, 2017 na 2018.

Chelsea ndio bingwa mtetezi wa kombe hili lakini ikashindwa kutetea ubingwa wake.

Fainali ya Kombe la Dunia ngazi ya klabu itachezwa Februari 11 mwaka huu jijini Rabat, Morocco. Madrid inashiriki michuano hii mara sita 2014, 2016, 2017 na 2018.

Chelsea ndio bingwa mtetezi wa kombe hili lakini ikashindwa kutetea ubingwa wake.

Mwanaspoti

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
1h ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
12h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
15h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
19h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
21h ago
READ MORE β†’