Klabu ya Simba imezindua jezi rasmi ambazo zitatumika katika mechi za hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Simba imeingia makubaliano na Bodi ya Utalii kuitangaza nchi kupitia nembo ya VISIT TANZANIA
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jezi hizo, Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally alisema M-Bet itaendelea kuwa Mdhamini Mkuu wa Simba katika michuano ya ligi ya mabingwa
Simba itavaa jezi zenye nembo ya VISIT TANZANIA katika mechi tu lakini inaposafiri itaendelea kuvaa jezi za Mdhamini Mkuu, M-Bet
Jezi mpya zitaanza kuuzwa rasmi Februari 15 na zitapatikana kwa Tsh 35,000/-



