Newcastle United itashindana na Manchester City katika kumsajili kiungo wa kati wa England James Maddison, 26, kutoka Leicester City. (Echo)
Manchester United wanapanga kutoa pauni milioni 100 kumnunua nahodha wa Tottenham ya Uingereza Harry Kane, 29, au mchezaji wa kimataifa wa Napoli mwenye umri wa miaka 24 Victor Osimhen, huku meneja Erik ten Hag akitaka mshambuliaji mwenye kiwango cha kimataifa. (Telegraph)
Wawekezaji wa Qatar hivi karibuni watatoa ofa rasmi kwa Manchester United ambayo wana uhakika itashinda mashindano yoyote, huku familia ya Glazer ikitaka kuiuza klabu hiyo kwa pauni 6bn. (Mail)
Manchester City wanataka kuzipiku Real Madrid na Liverpool katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa England Jude Bellingham mwenye umri wa miaka 19 kutoka Borussia Dortmund katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi - lakini tishio la kuwekewa vikwazo baada ya kushtakiwa na Ligi kuu England League linaweza kuwazuia kufanya hivyo. (Telegraph)
Borussia Dortmund wanaandaa ofa yao ili kumshawishi Bellingham kusalia Ujerumani kwa msimu mwingine. (90MIN)
Arsenal bado wanaweza kuamua kumuuza mchezaji wa kimataifa wa England Folarin Balogun msimu wa joto, licha ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kuongoza kwa mabao Ligue 1 akifunga mabao 14 katika mechi 21 akiwa na Reims msimu huu. (Sun)
Meneja wa Rayo Vallecano Andoni Iraola anafahamika kuwa miongoni mwa wagombea wakuu wanaowania kuchukua nafasi ya Jesse Marsch kama meneja wa Leeds United. (Independent)
Leeds United haitamteua meneja wao wa zamani Marcelo Bielsa au meneja wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino, ambaye anaifundisha Real Madrid. (Star)
Liverpool na Manchester United zote zimeanza kushughulikia mkataba wa majira ya joto kumnunua mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt mwenye umri wa miaka 24 Randal Kolo Muani. (L"Equipe, via Metro)
Mazungumzo ya Manchester United kuhusu kandarasi mpya na beki wa kulia wa Ureno Diogo Dalot yako katika hatua za mwisho, kumaanisha kuwa itakuwa vigumu kwa Barcelona kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Mundo Deportivo)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 27, ambaye alikaribia kujiunga na Manchester United mwaka jana, ni miongoni mwa wachezaji watano wa kikosi cha kwanza ambao watauzwa na Juventus. (Gazzetta dello Sport, via Mirror)
Inter Milan ilifanya mazungumzo na mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 35, kabla ya nyota huyo wa zamani wa Barcelona kuamua kujiunga na Paris St-Germain. (Goal)
Winga wa Roma ya Italia Nicolo Zaniolo mwenye umri wa miaka 23 amesafiri hadi Istanbul kukamilisha uhamisho wa kwenda Galatasaray. (Mail)
Kiungo wa kati wa Uhispania Sergio Busquets, 34, amepewa ofa ya mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya £16m kwa msimu na klabu ya Saudi Arabia Al Nassr lakini atasubiri kuona kama Barcelona itampa mkataba mpya kabla ya kufanya uamuzi. (Mundo Deportivo)
BBC