Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka nchini mapema kesho Alhamsi kuelekea Guinea kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Februari 11 huko Guinea, saa 1 usiku
Simba ilitanguliza watu wake Guinea kwa ajili ya kuweka sawa utaratibu na mapokezi ya timu
Simba itakuwa na siku moja ya kujifua kabla ya kuwavaa Horoya Ac siku ya Jumamosi katika mchezo ambao Simba inahitaji kushinda au hata sare