Yanga

Yanga yakamilisha maandalizi Tunisia

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Feb 2023
Yanga yakamilisha maandalizi Tunisia

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya US Monastir ambao utapigwa kesho Jumapili jijini Tunis

Aidha Nabi ameupongeza uongozi wa Yanga kwa kuipeleka timu mapema Tunisia, wamekuwa na muda mzuri wa kufanya maandalizi pamoja na kuzoea hali ya hewa

Nabi amesema wanakwenda kupambana na timu nzuri inayocheza soka la ushindi

"Nawashukuru viongozi wa Yanga kwa kuifikisha timu huku mapema kwa sababu ya hali ya hewa. Tumejiandaa vizuri, wachezaji wana ari kubwa"

"US Monastir ni timu ambayo inatoka sehemu nilipozaliwa, ni timu nzuri yenye upinzani lakini tumejiandaa vizuri, tutapambana kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri," alisema Nabi

Nae mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele amesema wanajua wanakwenda kupambana na timu nzuri, wachezaji wako tayari

"Sisi kama wachezaji tumejiandaa vizuri na tunajua tunakwenda kukutana na timu nzuri. Tupo tayari, tumekuja hapa kupambana, tutapambana mpaka mwisho"

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
2h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
6h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
6h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
7h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
8h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
8h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
9h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
9h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
23h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
23h ago
READ MORE β†’