Yanga

Nabi amtaka Feisal Yanga

Joel JJ By Joel JJ
13 Feb 2023
Nabi amtaka Feisal Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amemtaka kiungo Feisal Salum kufikiria hatma yake katika kusakata kabumbu kwa kufanya uamuzi sahihi

Feisal amekuwa nje ya uwanja tangu mwishoni mwa Disemba 2022 baada ya jaribio lake la kuvunja mkataba na Yanga kukwama

Pamoja na Mtendaji Mkuu wa Yanga Andre Mtine kumuandikia barua kumtaka aripoti Avic Town kuendelea na majukumu yake kwa mujibu wa mkataba, Feisal bado hajaonekana

Nabi alifanya mazungumzo na mchezaji huyo kupitia simu na kumshauri amalize mgogoro wake na Yanga ili aweze kurejea kwenye majukumu yake 

"Mimi ni baba namchukulia Fei au mchezaji yeyote niliyenaye kama mwanangu wa kiume Hedi, ukiangalia Yanga maisha yanaendelea, lakini maisha ya Feisal yamesimama na kipaji chake kimesimama"

"Nilimpigia, lakini niliongea na wachezaji wenzake nikamwambia kitu kikubwa sasa sio pesa tu anatakiwa pia kufikiria kuhusu kipaji chake, mtu bora ambaye atakuwa anamshauri vizuri ni yule atakayemwambia atafute nafasi ya kumaliza utofauti wake na klabu arudi kazini"

"Nafahamu athari za mchezaji kukaa nje bila kucheza mechi za mashindano, athari za mamna hiyo anaweza asizijue kwa undani mtu mwingine ambaye hachezi mpira wala hajacheza mpira, hata kama Feisal anataka kuondoka Yanga hiki kinachoendelea hakiwezi kumsaidia kitamuangamiza," Nabi alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

Hivi karibuni Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alisisitiza kuwa Feisal ni mchezaji wao mpaka May 2024

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
1h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
1h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
2h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
2h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
2h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
2h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
3h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
4h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
15h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
15h ago
READ MORE →