Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Mama Samia Suluhu ametangaza kununua kwa Sh5 milioni kila bao litakalofungwa na Yanga na Simba katika michezo yao ya michuano ya CAF mwishoni mwa wiki hii
Siku ya Jumamosi Simba itacheza na Raja Casablanca katika mchezo wa ligi ya mabingwa wakati siku ya Jumapili Yanga itacheza na TP Mazembe katika mchezo wa kombe la Shirikisho
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema ahadi hiyo ya Mh Rais ni sehemu ya motisha kwa wawakilishi hao wa Tanzania kuhakikisha wanapeperusha vyema bendera ya nchi katika mechi zao kwa kuibuka na ushindi
Kulingana na ratiba iliyotolewa na CAF mechi zote zitapigwa saa 1 usiku