PSG - Bayern - Tottenham - Brugge - Chelsea - Ac Milan

PSG ni yaleyale Ligi ya Mabingwa, yapigwa na Bayern

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Feb 2023
PSG ni yaleyale Ligi ya Mabingwa, yapigwa na Bayern

PSG wameshindwa kutamba nyumbani kwenye mchezo wa kwanza hatua ya 16 bora michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya wakikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Bayern Munich

Kingsley Coman ndiye aliyepeleka msiba PSG akifunga bao pekee la Bayern Munich katika ushindi huo muhimu wa bao 1-0 ugenini

Koeman ni mzaliwa wa Paris na kukulia PSG, Coman alifunga bao pekee wakati Bayern ilipoilaza timu ya Ufaransa kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa 2020 na akawa mfungaji pekee mabingwa hao wa Ujerumani walipotinga hatua ya robo fainali

Ni mechi ya tatu mfululizo PSG wanapoteza katika mashindano yote na sasa watakuwa na kazi ya ziada kwenye kusaka ushindi ugenini kule Munich

Katika mchezo mwingine uliopigwa jana, Ac Milan walianza vyema nyumbani kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspurs

Ac Milan walifunga bao pekee mapema tu kwenye dakika ya saba kupitia kwa Diaz katika mchezo ambao ulishuhudiwa na zaidi ya mashabiki 74,000

Pamoja na kupoteza mchezo huo Spurs inayonolewa na Antonio Conte ilicheza vyema hasa katika eneo la kiungo ambapo nyota wa Senegal Sarr mwenye umri wa miaka 20 alin'gara

Timu hizo zitarudiana baada ya wiki mbili nchini Uingereza

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
9h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
9h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
9h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
13h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
16h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
17h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
17h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
18h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
19h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
20h ago
READ MORE β†’