Mpaka sasa haifahamiki ni lini klabu ya Raja Casablanca itawasili nchini tayari kwa mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi
Katika Mkutano na wanahabari jana, Simba ilithibitisha kutokuwa na taarifa za ujio wa timu hiyo
Taarifa za ndani zimebainisha kuwa tayari timu hiyo imeondoka Morocco na huenda wakawasili nchini usiku wa leo
Mchezo baina ya timu hizi umeteka mijadala kwenye mitandao ya kijamii, hasa baada ya Raja kujibu andiko la Simba "Moto ni Ule ule kwa Mkapa hatoki Mtu"
Ni mchezo muhimu kwa Simba kutumia vyema uwanja wa nyumbani ili kujiweka katika nafasi nzuri katika mkakati wa kutinga robo fainali
Mchezo utapigwa saa 1 usiku ukitanguliwa na mchezo kati ya Vipers Fc dhidi ya Horoya Ac utakaopigwa saa 10 jioni huko Uganda
ADVERTISE HERE