Wapinzani wa Simba mchezo wa ligi ya mabingwa, Raja Casablanca iliwasili nchini mapema leo kuelekea mchezo wa pili kundi C ambao utapigwa Jumamosi, Februari 18 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Raja vinara wa kundi C baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Vipers, waliondoka Morocco jana wakipitia Doha Qatar na moja kwa moja kuunganisha nchini
Timu hiyo haikuweka wazi ujio wao kwa wenyeji wao klabu ya Simba iliyothibitisha Raja hawakuwapa taarifa juu ya siku ambayo watawasili
Nayo klabu ya TP Mazembe kutokea DR Congo imeanza safari kuja jijini Dar kwa ajili ya mechi ya pili hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Yanga
Mazembe ni kinara wa kundi D akiwa na pointi 3 baada ya kushinda mabao 3-1 dhidi ya Real Bamako atakutana na Yanga ambaye anasaka alama 3 katika kundi hilo baada ya mechi ya kwanza kuambulia kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa US Monastir ya Tunisia
Mechi hiyo itapigwa Jumapili Februari 19 saa 1 usiku.