Fc Barcelona jana ilishindwa kutamba katika uwanja wake wa Camp Nou ikilazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa ligi ya Europa hatua ya 16 bora
Barcelona walitangulia kufunga kupitia kwa Marcus Alonso kabla ya Marcus Rashford kusawazisha na kusababisha bao la pili ambalo mlinzi wa Barca Juoles Kunde alijifunga
Rafinha aliirejesha barca mchezoni kwa kuisawazisha katika dakika ya 76
Timu hizo zitarudiana tena wiki ijayo katika mechi itakayopigwa uwanja wa Old Trafford huko Uingereza