Transfer

Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi Februari 18 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 Feb 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumamosi Februari 18 2023

Manchester City wamefufua uoya nia yao ya kumnunua kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, 24. (90Min)

Liverpool wanashinikiza kumsajili kiungo wa kati wa England Mason Mount, 24 ambaye mazungumzo yake ya kuongeza kandarasi yake Chelsea yakisuasua (Mail)

Inter Miami ya David Beckham iko katika nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 35, iwapo ataamua kuondoka Paris St-Germain. (Mirror)

Lakini baba yake na Messi ambaye ni wakala wake pia, Jorge Messi, anasema hakuna uwezekano wa mchezaji huyo kurejea klabu yake ya zamani ya Barcelona tena. (ESPN)

Aston Villa wana nia ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Roma Muingereza Tammy Abraham, 25. (90min)

Leeds United wanaongoza katika mbio za kumsajili winga wa Canada Tajon Buchanan, 24, kutoka Club Bruges. (Calciomercato, via TeamTalk)

Chelsea bado hawajatuma maombi ya kibali cha kufanya kazi kwa ajili ya kiungo wake mpya wa kati wa Brazil Andrey Santos, 18, ambaye walimsajili mwezi Januari. (Athletic)

Juventus wameamua kumuuza kiungo wa kati wa Sweden Denis Zakaria mwenye umri wa miaka 26 akimaliza mmkopo wake Chelsea. (Standard)

Leeds wamemwambia bosi wao wa muda Michael Skubala, 40, kuwa anaweza kusalia kuinoa hadi mwisho wa msimu. (Min 90)

Newcastle United wanajiandaa kumpa mlinzi wa Uingereza Dan Burn, 30, mkataba mpya. (Football Insider)

Meneja wa Everton Sean Dyche anapanga kuangalia mtindo mzima wa maisha wa mshambuliaji wa England Dominic Calvert-Lewin, ikiwa ni pamoja na godoro analolalia, anapojaribu kukabiliana na masuala ya uimara wa kimazoezi na afya ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Times)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
37m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
49m ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
4h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
8h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
9h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
10h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
11h ago
READ MORE β†’