Yanga - Mazembe

Kocha TP Mazembe akiri, Yanga sio wepesi

Joel JJ By Joel JJ
18 Feb 2023
Kocha TP Mazembe akiri, Yanga sio wepesi

Kocha Mkuu wa TP Mazembe Mihayo Kazembe amesema mchezo wao wa kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili, Februari 19 utakuwa mgumu

TP Mazembe walitua nchini Alhamisi jioni tayari kwa mchezo huo ambapo jana Ijumaa walifanya mazoezi yao ya mwisho katika uwanja wa Benjamin Mkapa ambao utatumika siku ya Jumapili

Kazembe amesema wanafahamu Yanga ina wachezaji wazuri ambao miongoni mwao wametoka DR Congo

"Yanga ni timu nzuri na yenye wachezaji wazuri, katika kikosi cha Yanga kuna wachezji wengi tu wazuri na wenye uwezo mkubwa wa kucheza mpira na kufanya maamuzi. Tunafahamu wachezaji wao baadhi ni Wacongo"

"Mchezaji kama Aziz Ki na hata Fiston Mayele ni wachezaji ambao wana majina makubwa na wanafanya vizuri tunaamini mechi haitakuwa rahisi lakini tumekuja hapa kushindana, muhimu kutafuta alama muhimu ugenini" alisema Kazembe

Kuelekea mchezo huo, Yanga inanufaika kwa kuwa na idadi kubwa ya wachezaji kutoka DR Congo ambao wamewahi kucheza dhidi ya TP Mazembe wakiwa na klabu ya AS Vita

Wachezaji kama Yannick Bangala, Djuma Shaban, Jesus Moloko, Tuisila Kisinda, Fiston Mayele na Joyce Lomalisa wamewahi kuitumikia AS Vita kabla ya kusajiliwa na Yanga

TP Mazembe ndio vinara wa kundi D wakiwa na alama tatu baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Real Bamako

More Stories

Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
52m ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
55m ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
1h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
1h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
1h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
3h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
13h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
13h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
14h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
17h ago
READ MORE →