Simba

Simba itaendeleza utamaduni dimba la Mkapa?

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 Feb 2023
Simba itaendeleza utamaduni dimba la Mkapa?

Muda unazidi kuyoyoma, majira ya saa 1 usiku Simba itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Raja Casablanca katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika

Ni mchezo wa pili kundi C, mchezo ambao unaweza kutoa taswira ya matumaini ya Simba katika mkakati wa kusonga mbele hatua ya robo fainali

Ni moja kati ya mechi tatu ambazo Simba watacheza uwanja wa nyumbani katika michuano hiyo, lengo likiwa kukusanya alama tisa

Mashabiki wa Simba hawajawahi kuwa na hofu na timu yao pale inapocheza uwanja wa Benjamin Mkapa

Sawa, ziko mechi chache ambazo Simba haikushinda nyumbani lakini mechi nyingi katika michuano ya ligi ya mabingwa, Mnyama aliunguruma dimba la Mkapa

Mashabiki wa Simba wanakwenda dimba la Mkapa wakiwa na matumaini makubwa kuwa timu yao leo itaendeleza rekodi yake ya kutumia vyema uwanja wa nyumbani katika michuano ya ligi ya mabingwa

Ni mechi muhimu sana kwa Simba kushinda, ikumbukwe Wekundu hao wa Msimbazi walipoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Horoya Ac uliopigwa Guinea

Kuelekea mchezo huo, Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema kuwa pamoja na kuwa mpira una matokeo matatu lakini leo wanahitaji tokeo moja tu, ambalo ni ushindi kwa Simba

"Leo kuna mambo mawili lazima yatokee uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba kuifunga Raja Casablanca au Raja Casablanca kufungwa na Simba!," ni kauli ya shabiki kindakindaki wa Simba aliyejitambulisha kwa jina moja Rashid alipokuwa akitamba wakati akielekea dimba la Mkapa

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
34m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
46m ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
4h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
8h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
9h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
10h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
11h ago
READ MORE β†’